Mwanasoka nguli kutoka Argentina na klabu ya PSG Lionel Messi ametangazwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka 2022 FIFA, huku akiweka rekodi ya kuwa Mchezaji pekee aliyewahi kuingia kwenye kikosi bora cha FIFA cha mwaka mara nyingi zaidi 16 akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyeingia mara 15.
Tuzo hii ya Messi alikuwa anawania na Wakali wengine kama Karim Benzema pamoja na Kylian Mbappe.
Tuzo nyingine zilizotolewa usiku wa kuamkia leo katika usiku wa tuzo za FIFA (FIFA The Best) ni tuzo ya golikipa bora iliyokwenda kwa golikipa wa Argentina na Aston Villa Emi Martinez.
Tuzo ya Kocha bora imeenda kwa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Scaloni, tuzo ya kikosi bora cha mwaka zikibebwa na Courtois, Hakimi, Cancelo, Van Dijk, Modric, De Bruyne, Casemiro, Messi, Benzema, Haaland na Mbappe.
Leave a Reply