Messi azungumzia kustaafu kwake

Messi azungumzia kustaafu kwake

Licha ya kuwa mchezaji wa Inter Miami Lionel Messi, atafikisha miaka 37 mwezi Juni, amefunguka kuwa atastaafu soka, muda ambao atahisi hawezi tena kufanya vizuri zaidi kwenye soka.

Akizungumza na Big Time Podcast ya MBC, fowadi huyo wa Inter Miami na Argentina alisema atajua ni lini wakati muafaka wa kuondoka kwenye mchezo huo.

"Ninajua mara tu ninapoamini kwamba siwezi tena kucheza, au kufurahia mchezo tena, au kutokuwa na uwezo wa kusaidia wachezaji wenzangu, basi nitaacha".

Ninajikosoa sana, najua ninapokuwa mzuri au mbaya, ninapocheza vizuri na vibaya, nikihisi ni wakati wa kuchukua hatua hiyo, nitaichukua bila kufikiria."Alisema Messi

Ikumbukwe kuwa mkataba wa Messi na Inter Miami unamalizika Desemba 2025. Kumekuwa na uvumi kwamba huenda akamaliza soka na Newell's Old Boys, klabu ya Argentina aliyoichezea akiwa mvulana kabla ya kujiunga na Barcelona.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudkaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post