Messi atoa Iphone  kwa wachezaji wenzake wa Argentina

Messi atoa Iphone kwa wachezaji wenzake wa Argentina

Aloooooweeeh! Aloootenaaa! Sijui tuseme wiki hii ni wiki ya mwamba La Pulga au Messi kuupiga mwingi kwa kuwazawadia wachezaji wake na benchi la ufundi kwa kuwapatia simu za iphone.

Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Argentina na Klabu ya PSG  Leone Messi ametoa ya Simu 35 aina ya iPhone 14 ambazo zimewekewa cover za dhahabu kwa wachezaji wote na Benchi la Ufundi ikiwa ni zawadi kwa ushindi wa Kombe la Dunia.

Ikumbukwe tuu timu hiyo ilitwaa ubingwa huo Disember 18, mwaka 2022 baada ya kulisaka Zaidi ya miaka 15. Nyie nyie haya dondosheni komenti hapo chini tufikirie wote kwa sauti kuna mchezaji hata mmoja kashawaitoa hata tekno hahahaha! Jokes.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags