Messi ashambuliwa mtandaoni kisa Pizza

Messi ashambuliwa mtandaoni kisa Pizza

Star wa ‘klabu’ ya #InterMiami #LionelMessi amejikuta akirushiwa maneno na mashabiki mtandaoni baada ya ku-post picha ya Pizza aliyokuwa anataka kuila.

‘Staa’ huyo ameonesha kiwango bora tangu msimu huu uanze ambapo amefunga mabao matano na kutoa ‘asisti’ 11 kwenye ‘mechi’11.

Messi aliamua kujikumbushia chakula cha nyumbani kwao Argentina, kwa kula Pizza iitwayo Argentine pizzeria Banchero ambayo ni maarufu nchini Argentina. Aliagiza kwa ‘oda spesho’ kwenye moja ya maduka ya pizza Jijini Miami anakoishi sasa.

Lakini baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram mashabiki walishangazwa na jinsi ilivyokuwa ikionekana tofauti na Pizza nyingine walizozoea.

Kwa mujibu wa The sun inadai kuwa mmoja ya mashabiki ali-comment kwa kudai "Pizza mbaya kuwahi kuishuhudia", huku watu wengine wakiendelea ku-comment Maneno mabaya dhidi ya pizza hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags