Messi aanza vizuri Inter Miami

Messi aanza vizuri Inter Miami

Usiku wa kuamkia leo ‘klabu’ ya Inter Miami kutoka nchini Marekani ilikuwa na mchuano ya kucheza na ‘timu’ ya Cruz Azul kwenye mchezo wa Leagues Cup, mashindano yanayozikutanisha ‘klabu’ za kutoka Ligi Kuu ya Marekani dhidi ya ‘klabu’ za Ligi ya Mexico ifahamikayo kama Liga Mx.

La Pulga ameanza msimu kiaina yake kwa kupachika ‘goli’ katika ‘klabu’ hiyo kwenye dakika za nyongeza, jambo ambalo mashabiki wa ‘timu’ hiyo hawakutegemea.

Messi alitambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Inter Miami Julai 16 baada ya kuachana na ‘klabu’ ya PSG.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags