Mercy: Mpenzi wangu alinipa zaidi ya milioni 300 nikazikataa

Mercy: Mpenzi wangu alinipa zaidi ya milioni 300 nikazikataa

Mwigizaji, mfanyabiashara, video vixen  na mshindi wa Big Brother Naija 2019 Mercy Eke kutoka nchini Nigeria, ameweka wazi kuwa alikataa ‘ofa’  ya N120 milioni ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh 300 milioni alizopewa na mpenzi wake ili asishiriki shindano la Big Brother All Star msimu mpya wa 2023.

Mercy ameweka wazi kukataa pesa hizo wakati akizungumza na mshiriki mwenziye kwenye mjengo wa BBN, Princess Francis, Mercy alidai kuwa mpenzi wake huyo alitaka kumpatia zaidi ya Tsh 300 milioni kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kutoshiriki msimu mpya ambao unahusisha washiriki maarufu  wa misimu tofauti iliyopita.

Mercy Eke ndiye alikuwa mwanamke wa kwanza kushinda shindano la Big Brother Naija mwaka 2019 na aliondoka na zawadi mbalimbali ikiwemo kiasi cha pesa cha zaidi ya Tsh 100 milioni. Kwa sasa mashindano hayo ya Big Brother Naija All Star, yamejumuisha washiriki wa miaka tofauti ya nyuma iliyopita, huku Mercy akidai kuwa amekataa pesa kutoka kwa mpenzi wake kwani anaamini atashinda tena, na atapata fursa nyingi zaidi ya pesa.

Ungekuwa wewe ungekata hizo pesa?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags