Meneja akanusha taarifa ya bondia Deontay Wilder kustaafu

Meneja akanusha taarifa ya bondia Deontay Wilder kustaafu

Bondia Deontay Wilder bado ameendelea kuwa kimya juu ya hatma yake kwenye masumbwi tangu alipoahidi endapo atachapwa na Zhilei Zhang, nchini Saudi Arabia, atastaafu.

Wilder aliyewahi kushikilia mkanda wa WBC kwa zaidi ya miaka mitano kabla ya kuuachia mkanda huo kwa Tyson Fury mwaka 2021, aliahidi kustaafu ngumi kama atapigwa na Zhilei na alichapwa vibaya, huku wengi wakisubiri atangaze kustaafu, ukimya umetawala.

Jana Jumatatu, kuliibuka taarifa mpya ya bondia huyo Mmarekani ameshaamua kujiweka pembeni kuhusu ngumi kiasi cha kumfanya meneja mwenza wa bondia huyo, Shelly Finkel kupingana na taarifa hizo akisisitiza bado hajaambiwa uamuzi huo na Wilder.

Tayari Wilder ameshaporomoka kwenye orodha ya ubora wa WBC kutoka namba moja aliyowahi kuwa hadi namba 15 na kwa hali ilivyo, kama hatapigana karibuni na kushinda pambano kubwa, atazidi kuporomoka zaidi na kutimiza mwisho wake wa kuzichapa ulingoni. Wilder anatajwa kutamani siku moja apigane na Oleksandr Usyk kabla ya kuacha ngumi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags