Megan apata shavu Warner Music

Megan apata shavu Warner Music

Ni mwezi mmoja umepita tangu ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Megan Thee Stallion kutemana na ‘lebo’ yake ya zamani ya ‘1501 Certified Entertainment’, hatimaye kwa sasa amelamba dili nono katika Kampuni ya ‘Warner Music Group’ itakayofanikisha kusambaza kazi zake za muziki.

#Megan alitemana na ‘lebo’ hiyo kisheria kufuatiwa na kutoelewana na uongozi huku akidai kuwa alikuwa akizuiliwa kutoa nyimbo.

Na sasa 'amesaini' na ‘Warner Music Group’ kampuni inayomilikiwa na Bilionea #LeonardBlavatnik ambayo inaupiga mwingi kwenye kupelea muziki kimataifa.

#MeganTheeStallion anatamba na ngoma zake zikiwemo ‘Sweetest Pie’, ‘Her’, ‘Cobra’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags