Meek Mill: Jay-z alinifundisha namna ya kufunga kamba za viatu

Meek Mill: Jay-z alinifundisha namna ya kufunga kamba za viatu


‘Rapa’ kutoka Marekani Meek Mill ameweka wazi kuwa hapo mwanzo alikuwa hajui kabisa kufunga Kamba za viatu lakini alifundishwa na ‘rapa’ tajiri zaidi nchini humo Jay-Z.

Kupitia na video inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii Meek Mill amesikika akisema miaka kadhaa iliyopita alikuwa hajui kabisa kufunga Kamba za viatu huku akimtaja Jay-Z kuwa ndio mtu wa kwanza ambaye kumfundisha namna ya kufunga kamba za viatu aina ya ‘Timberland’.

Utakumbuka kuwa wawili hao walianza urafiki miaka mingi iliyopita ambapo pia wamewahi kufanya ‘kolabo’ za pamoja ikiwemo ‘What's Free’, ‘Big Dreams’, ‘Dont Believe In Dreams’ na nyinginezo.

Mbali na kufanya ‘kolabo’ nyingi pamoja pia Jay-Z aliwahi kumtetea Meek Mill aweze kuachiwa huru kwa kumtolea dhamana kufuatia na kesi iliyokuwa ikimkabili miaka michache iliyopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags