Mchungaji afariki alipojaribu kufunga kwa siku 40 kama Yesu

Mchungaji afariki alipojaribu kufunga kwa siku 40 kama Yesu

Mchungaji kutoka nchini Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga siku 40 akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu kwenye Mlima wa Mizeituni wa Biblia.

Kifo cha mchungaji  Francisco Barajah, ambae pia ni mwanzilishi wa Kanisa la Kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica, walithibitishwa Jumatano.

Muchungaji huyo alifariki alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishwa akiwa katika hali mbaya. Baada ya siku 25 za kufunga, alikuwa amepungua uzito sana hadi hakuweza kusimama, kuongea wala kutembea.

Siku kadhaa baadaye kwa msisitizo wa ndugu na waumini, alipelekwa hospitalini lakini jitihada za kumrejesha kwenye afya hazikufaulu.

Waumini wa kanisa lake na majirani zake hawakushangazwa na mabadiliko hayo, kutokana na kupungua uzito na umbo lake kuharibika katika siku za hivi karibuni.

Chazo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags