Mchekeshaji Molingo afariki dunia Chato
Mchekeshaji Frank Patrick 'Molingo' Mkazi wa Wilaya ya Chato mkoani Geita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 10,2024.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Mudi Msomali, aliyekuwa akiishi naye na kumsimamia katika Sanaa yake.
"Inalilahi wainalilahi rajiun nimepambana imeshindikana. Pumzika kwa amani Molingo kwa yeyote atayeguswa na msiba usiache kuwasupport kwao kwa chochote kesho tumsitili Molingo,"ameandika Mudi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo taarifa rasmi ya kilichosababisha kifo chake bado hazijatolewa. Utakukumbuka enzi za uhai wake Molingo (17) alikuwa akionekana kwenye video mbalimbali akichekesha na mwenziye Mudo, huku vichekesho vyao vingi vikiwa vya kubishana.
Mwananchi ilipomtafuta Msomali kuzungumzia hilo alijibu mara moja baada ya salamu kuwa ni kweli amefariki ila anaomba atafutwe baadae kidogo.
Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari kamili.
Leave a Reply