Mc Pilipili amwaga maua kwa Conboi

Mc Pilipili amwaga maua kwa Conboi

Na Masoud Kofii

Mchekeshaji na mshehereshaji Mc Pilipili ameonesha mapenzi yake kwa msanii wa hip-hop nchini Conboi Cannabino baada ya kukutana nae kwa mara ya kwanza.

Katika kuonesha furaha hiyo Pilipili amesema Conboi ndiye msanii wake pendwa aliyekuwa akiota kukutana nae.

"Leo mimi ni kama zile ndoto mtu anaomba akutane na Diamond au msanii mkubwa, kiukweli uandishi wako unakufanya kukaa vichwani mwa watu. Hapa katikati nilipitia vitu vigumu sana anguko kubwa lakini wimbo wako wa 'Till I Die' ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya nirudi kwenye gemu ya komedi," amesema MC Pilipili kwenye video iliyochapishwa na Conboi kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo Pilipili amezungumzia namna wimbo wa 'Till I Die' ulivyomuinua na kumbariki licha ya kuwa sio wimbo ya injili

"Tuna kawaida ya kujua unaweza kuinuliwa na wimbo wa gospel lakini Mungu sio binadamu anaweza kumtumia yeyote akaandika wimbo kwa ajili yako nilimcheki dogo mmoja anaitwa Jolmasta ambaye ni mchekeshaji pia kanambia huu ni wimbo wake bora sana," amesema Mc Pilipili






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags