Mbosso: Sina ugomvi na Abdukiba

Mbosso: Sina Ugomvi Na Abdukiba

Waja waja waja nawaita mara tatu msigombanishe watu wawatu jamani hahhahha!, staa wa muziki nchini King Khan Mbosso mwenyewe kupia mahojiano yake na chombo cha habari cha bosi wake aliulizwa swali bwana kuhusiana na yeye na Abdu Kiba kuwa katika ugomvi, kuwa wawili hao wakihusishwa na stori za kuchukuliana wanawake, kuwa Mbosso amezaa na aliekuwa mke wa Abdukiba

Mbosso alifunguka kuhusiana na swali aliloulizwa na kujibu kuwa “Labda huko zamani ilikuwa kwa bakati mbaya kwasababu tulikuwa hatujui na dada zetu kama mnavyo wajua huwa hawasemagi, unajua zinavyokuja habari huwa zinakuja kwa njia tofauti tofauti labda ndo njia ya kutugombanisha” amesema Mbosso Khan

Duuuuuuuu! Kumbe kuna siri kama hizi na hamsemi binadamu mna siri sana kwakweli, usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii mtu wangu wa nguvu @Mwananchiscoop.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post