Mbosso akubali uwezo wa Kipre Junior

Mbosso akubali uwezo wa Kipre Junior


Mwanamuziki wa bongo fleva #Mbosso ameukubali uwezo wa mchezaji kutoka ‘Klabu’ ya Azam #KipreJunio baada ya kupiga hat-trick jana katika mcheza wao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mbosso kupitia Instastory yake ame-share video ya goli la tatu la #Kipre na kueleza kuwa watu wanamchukulia poa mchezaji huyo ila ndiye winger pekee kwenye Ligi ya #Tanzania mwenye uwezo wa kukupa kila unachotaka kwa wakati sahihi anapokuwa uwanjani.

‘Mechi’ hiyo ya Azam na Mtibwa Sugar ilitamatika kwa mabao 5-0 huku mchezaji huyo akiondoka na mpira baada ya kufunga mabao matatu (hat-trick).

Unaungana na Mbosso kwenye kauli hii?.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags