Mbinu ya kuskiliza voice note, bila watu wa pembeni kuskia kitu

Mbinu ya kuskiliza voice note, bila watu wa pembeni kuskia kitu

Wapo baadhi ya watumiaji wa mtandao wa WhatsApp wamekuwa wakipata shida kusikiliza Voice Note wanazotumiwa wakiwa mbele za watu kwa kuhofia jumbe zao kusikiwa na watu wa pembeni, bila ya kufahamu kuwa ipo njia nyepesi ya kusikiliza Voice Note bila ya walio pembeni kusikia kitu.

Mtumiaji wa WhatsApp endapo utatumiwa ujumbe kwa njia ya Voice Note ukiwa mbele za watu na hauna #EarPhones, bado unanafasi ya kusikiliza ulichotumiwa bila ya wengine kusikia kitu, unachotakiwa kufanya ni kufungua sauti uliyotumiwa na kisha kuweka simu sikioni kama unazungumza na mtu, kwa kufaya hivyo sauti unayosikiliza haitafika kwa watu wengine badala yake itasikika tu kwenye spika ya mbele na utaisikia wewe pekeyako.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post