Mayweather kutuma ndege yake israel

Mayweather kutuma ndege yake israel

Bondia mstaafu ambaye pia ni ‘promota’ wa mchezo wa ngumi kutoka nchini Marekani ameonesha kuguswa na vita inayoendelea kati ya Israel na Palestina hivyo basi amepanga kutuma ndege yake binafsi ili kupeleka vifaa nchini Israel.

Kwa mujibu wa TMZ inaeleza kuwa Floyd atashirikiana na shirika la kutoa misaada nchini Israel ambapo amepanga kutumia Air Mayweather kupeleka vifaa kama vile chakula, maji na ‘vesti’ zisizoingia risasi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa bondia huyo hakuweka wazi taarifa hiyo ya kutoa msaada ‘ali-share’ ‘picha’ ya bendera ya nchi hiyo huku akiambatanisha na ujumbe usemao,

“Ninasimama na Israeli na Wayahudi kote ulimwenguni. Ninalaani chuki dhidi ya Wayahudi kwa gharama yoyote ile, ninasimama kwa ajili ya Amani, ninasimamia haki za kibinadamu, ugaidi siyo jibu Kamwe.”

Ikumbukwe siyo mara ya kwanza kwa Floyd kutoa msaada katika wakati wa maafa, miezi michache iliyopita alisaidia familia 70 kwa kuwapatia chakula, makazi na usafiri baada ya moto wa Maui.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags