Mayele: Nitarudi tena yanga, ni familia yangu

Mayele: Nitarudi tena yanga, ni familia yangu

Baada ya zile sintofahamu za mashabiki dhidi ya hatima ya Ferston Mayele kuwepo katika ‘klabu’ ya #Yanga hatimae zimefikia kikomo baada ya ‘klabu’ hiyo kufanya maamuzi na kumpa ‘thank you’ kwa kufikia makubaliano na ‘klabu’ ya Pyramids FC kumnunua mchezaji wao Mayele.

Lakini kupitia kurusa wa Instagram ya ‘klabu’ ya #Yanga Mayele ametoa shukurani za dhati kwa mashabiki wake na ‘timu’ kwa ujumla, hakusita kumsifia engeneer Hersi Said kwa kuwa na roho ya kiungwa katika ‘klabu’,  Mayele amesema,

“Uamuzi niliochukua ulikuwa mgumu sana haikuwa rahisi ila naishukuru ‘klabu’ yangu ya #Yanga nilipokelewa vizuri nilikuwa naishi kama niko kwetu,

“Tulikaa sana na viongozi wanilinipamabania ni baki lakini ikawa ni ngumu niliwaambia nataka kwenda kutafuta changamoto nyengine leo kesho nitarudi nyumbani kwa sababau #Yanga ni familia sio rahisi kumsahau engeneer Hersi Said anaishi na wachezaji vizuri sana na kutatua changamoto za wachezaji kambini”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags