Maxi apewa gari

Maxi apewa gari

Ma-bosi wa ‘klabu’ ya #Yanga wamempa zawadi ya gari mchezaji #MaxiNzengeli mara baada ya ‘kiungo’ huyo kupiga mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars kwa lengo la kumpandisha mzuka zaidi kufuatia ‘mechi’ ya watani wa jadi.

Maxi alikabidhiwa gari aina ya #ToyotaCrown baada ya ma-bosi wa ‘klabu’ kuvutiwa na kiwango ambacho ameendelea kukionesha huku wakieleza kuwa pia ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili.

Mchezaji huyo amezungumzia mechi dhidi ya #Simba na kusema ni miongoni mwa mchezo wenye presha na mgumu kwani zinakutana timu kubwa zenye ushindani na ubora hivyo macho ya watu yanatamani kuona nini kitakwenda kutokea na wao wamejipanga kufanya jambo.

“Huu ni mchezo mkubwa utakaotazamwa sana hivyo kila mchezaji anatakiwa kucheza kwa juhudi kubwa na morali ili kuweza kufanikiwa katika mechi hiyo yenye ushindani mkubwa,”alisema #Maxi huku akionyesha kuwa na mzuka wa mchezo huo ambao #Simba ni wenyeji.

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili, Novemba 5.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags