Mawaziri kulinogesha tamasha la Faraja Ya Tasnia

Mawaziri kulinogesha tamasha la Faraja Ya Tasnia

Mawaziri watano sambamba na Mshauri wa Rais, Angellah Kairuki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wanatarajiwa kushiriki Tamasha la Faraja ya Tasnia litakalofanyika kesho Jumamosi  September 7, 2024 kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Mwananchi, muandaaji wa tamasha hilo, Steve Nyerere amewataja mawaziri watakaoshiriki tamasha hilo la kuwakumbuka wasanii marehemu ni; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa na Angellah Kairuki.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro, Naibu wa Wizara hiyo, Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na Mshauri wa Rais Angellah Kairuki.

Tamasha hilo litakuwa la kwanza nchini kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki na Steve Nyerere  ameliambia Mwanaspoti, litakuwa linafanyika kwa mwaka mara moja bila ya kuweka kiingilio.

Steve Nyerere amesema, mbali na kufanyika maombi katika tamasha hilo, kutakuwa pia na burudani za  muziki ambapo baadhi ya wasanii wamejikusanya na kuimba wimbo wa pamoja, na wasanii wengine  watatoa burudani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags