Mawakili Megan wakanusha tuhuma zinazomkabili msanii huyo

Mawakili Megan wakanusha tuhuma zinazomkabili msanii huyo

Timu ya wanasheria wa Megan Thee Stallion inakanusha vikali madai yaliyotolewa na mpiga picha wa zamani wa msanii huyo Emilio Garcia kuhusiana na unyanyasaji wa kihisia na mazingira magumu ya kazi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Rolling Stone mawakili wa Megan, Mari Henderson na Alex Spiro, waliwasilisha hati mahakamani ikidai kuwa madai ya unyanyasaji wa kihisia yaliyotolewa na mpiga picha huyo hayana ukweli wowote.

Aidha katika nyaraka hizo zilieleza kuwa Garcia ni mlaghai ambaye anaidanganya mahakama ili aweze ku-trend na kukuza taaluma yake ya uimbaji iliyofeli ambapo kwa sasa anajaribu kutumia jina la Megan vibaya ili kurudi tena mjini.

Ikumbukwe kuwa April mpiga picha Garcia alifungua mashitaka dhidi ya Megan kwa kudai kuwa Juni 2020 Megan alimlazimisha amtazame akiwa anafanya ngono katika gari kisha baada ya tukio hilo alimuonya kuwa asiseme chochote alichoshuhudia ili kulinda heshima ya rapa huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags