Mavokali na Madee watia neno video ya Rayvanny

Mavokali na Madee watia neno video ya Rayvanny

Baada ya mwanamuziki Rayvanny ku-post video yake ikionesha umati wa watu waliokusanyika #Albania kwa ajili ya kushuhudia performance yake, Mavokali na Madee watia neno kwenye video hiyo.

Mavokali ame-comment kwenye video hiyo na kudai kuwa anadhani watu wanajionea sasa sababu yaye kufanya remix na chui. Ikumbukwe kuwa wawili hao walifanya remix ya wimbo wa Mavokali ulioenda kwa jina la commando (mapopo).

Mavokali ameandika,
“Alafu mtu anatokea anasema why umefanya remix na chuiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nadhani wanajionea πŸ™ŒπŸ”₯πŸ”₯ congrats brother.”

Mkongwe wa muziki @madeeali naye hajakaa kimya katika video hiyo ametupia comment yenye utani ndani yake akidai kuwa majirani zetu kutoka Kenya wakiona video hiyo yenye umati wa watu wakimshangilia Chui basi watadai kuwa Vanny anatokea Kenya na sio Mbeya.

Madee ameandika,
“wakenya wakiona hii watasema wewe wa kwao...sio wa Mbeya... Congr Tiger”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags