Mauzo ya tiketi za pambano la Jake na Tyson ni kufuru

Mauzo ya tiketi za pambano la Jake na Tyson ni kufuru

Imeripotiwa kuwa pambano la ndondi kati ya Jake Paul na Mike Tyson limefanya kufuru katika mauzo yake ya ‘tiketi’ baada ya kupata dola milioni 10 ikiwa ni zaidi ya Sh 25 bilioni, katika mauzo ya tiketi kwa siku ya kwanza.

Wawili hao wanatarajia kuoneshana ubabe Julai 20, 2024 katika uwanja wa AT&T, pamoja na pambano hilo kuoneshwa moja kwa moja (live) katika mtandao wa Netflix.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mabondia hao walitoa bei ya tiketi za VIP ambapo ‘tiketi’ moja inagharimu kiasi cha dola 2 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 5 bilioni.

Ambapo ukinunua ‘tiketi’ hiyo utafanikiwa kupata huduma za kipekee ambazo ni kupiga picha na mabondia hao kabla ya pambano kuanza, kupewa glavu zilizosainiwa na mabondia, chumba cha faragha chenye huduma ya hali ya juu, pia utapata fursa ya kupanda jukwaani wakati wa upimaji uzito wa mabondia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags