Master J atoa shukrani kupata shavu BASATA

Master J atoa shukrani kupata shavu BASATA

Producer maarufu nchini Master J ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Baraza Na.23 ya mwaka 1984 sura 204.

Baada ya uteuzi huo Master J kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa shukrani zake kwa waziri Ndumbaro, kwa kumteua kuwa mjumbe, na kuahidi kutimiza wajibu wake kwa uadilifu na weledi kwa ushirikiano na wajumbe wenzake.

 Huku ‘mastaa’ wengine walioteuliwa katika baraza hilo ni Single Mohamed Mtambalike (Richie Richie), Jessica Julius Mshama, Dkt. Gervas Andrew Kasiga (Chuma), Felista Steven Lelo na Mgunga Attilio Mwamnyenyerwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags