Mastaa Chelsea wajiondoa kwenye mtandao wa X

Mastaa Chelsea wajiondoa kwenye mtandao wa X

Wachezaji wa ‘klabu’ ya #Chelsea,  #MoisesCaicedo na #EnzoFernandez wamefuta akaunti zao za  X (Twitter) baada ya kupokea jumbe nyingi zilizokuwa na kauli za unyanyasaji na chuki baada ya ‘timu’ hiyo kufungwa na ‘klabu’ ya Liverpool.

Jumbe hizo walianza kuzipokea baada ya mchezo kutoka kwa mashabiki wa Chelsea waliochukizwa na matokeo hayo ndipo walipoa amua kuchuka hatua hiyo.

Hata hivyo Gazeti la The Sun lilijaribu kuitafuta ‘klabu’ hiyo kwa kujua undani wa wachezaji hao walio jiunga na Chelsea mwaka jana lakini walikataa kusema chochote.

‘Klabu’ ya Chelsea ilifungwa mabao 4-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Anfield, siku ya jumatano.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags