Mastaa Bongo Waivamia Nigeria Kumuunga Mkono Jux Na Mkewe

Mastaa Bongo Waivamia Nigeria Kumuunga Mkono Jux Na Mkewe

Baadhi ya watu maarufu kuokea nchini wamefunga safari kwenda nchini Nigeria kwaajili ya kumuunga mkono msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux na mkewe Priscilla ambao wanatarajia kufunga ndoa ya kimala hapo kesho Aprili 17, 2025.

Mastaa ambao tayari wamewasili nchini humo ni pamoja na msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz, Jimmy Chansa, Poshy Queen, Mc Garab, pamoja na familia ya msanii Juma Jux.

Harusi hiyo ya kitamaduni ni moja kati ya mfululizo wa zile sherehe za baada ya ndoa yao iliyofanyika Februari 7, 2025. ambapo alitangaza kuzifanya mwaka huu nchini Nigeria na Tanzania.



Baada ya harusi hiyo ya kitamaduni Jux na mkewe wanatarajia kufanya tafrija nyingine Mei mwaka huu nchini ambapo itahusisha ndugu, jamaa, Marafiki, mashabiki na watu wengine wa karibu.

Hata hivyo, Jux na mke wake wamekuwa Nigeria tangu Machi, ambapo walihudhuria uzinduzi wa filamu ya Labake Olododo ambayo imechezwa na mama mzazi wa priscilla, Iyoboojofespris.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags