Mashemeji wacharuka, Wadai kanye anamchukulia mkewe kama mradi

Mashemeji wacharuka, Wadai kanye anamchukulia mkewe kama mradi

Baada ya mwanamuziki KanyeWest na mkewe Bianca Censori kutokuwa kwenye maelewano mazuri kwa hivi karibuni, marafiki wa mwanamke huyo wanadai kuwa Kanye anamchukulia mkwewe kama mradi wa sanaa.

Marafiki hao kutoka nchini Australia wamefichua kuwa Bianca anafanywa kama mradi wa sanaa na biashara kwa kuvaa mavazi yasiyofaa wakati akiwa na Kanye.

Aidha tovuti ya Times Now imeeleza kuwa baadhi ya watu wanamuona Bianca kama amerukwa na akili kutokana na kufuata sheria za mumewe hasa kwenye mavazi.

Hata hivyo baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii walidai kuwa mwanamke huyo alilazimishwa na Kanye kuvaa mavazi ya kuacha nusu ya mwili wake wazi.

Ikumbukwe kuwa rapper huyo mwenye umri wa miaka 46, alimuoa Bianca mwaka 2022, muda mfupi baada ya kuachana na Kim Kardashian.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags