Mashabiki wataka kufahamu hali ya mwanasoka Merritt

Mashabiki wataka kufahamu hali ya mwanasoka Merritt

Mashabiki wa South Sydney nchini Australia wavunja ukimya wao kwa kutaka kujua kuhusu hali ya mwanasoka  Nathan Merritt anayepigania maisha yake hospitalini baada ya kutokuwa na taarifa za maendeleo ya star huyo.

Nyota huyo wa zamani wa ‘klabu’ #SydneyRabbitohs mwenye umri wa miaka 40, alikimbizwa katika Hospitali ya Royal Prince Alfred iliyoko magharibi mwa Sydney na kuwekwa kwenye uangalizi siku ya Ijumaa baada ya kugundulika ameathirika na dawa za maumivu.

Baba huyo wa watoto watano inadaiwa kuwa na athari mbaya kwa kutumia dawa za maumivu alizopewa na kudhani zitamponya maumivu yaliokuwa yanamsumbua, lakini aliishia kupoteza fahamu nyumbani kwake.

Hata hivyo imeonekana kuwa Merritt alishiriki katika hafla ya Koori Knockout iliyofanyika The Central Coast ‘wiki’ iliyopita ambapo inadaiwa alionekana kupata mshtuko  wa moyo akiwa katika sherehe hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags