Mashabiki wasusia tamasha, Baada ya mchekeshaji kuongelea vita ya Islael, Palestina

Mashabiki wasusia tamasha, Baada ya mchekeshaji kuongelea vita ya Islael, Palestina

Mchekeshaji kutoka nchini #Marekani, #DaveChappelle amejikuta akiwafukuza mashabiki walio hudhuria katika tamasha lake la vichekesho baada ya kuongelea mgogoro wa Islael na Palestina huko TD Garden Boston.

 Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa Dave aliongelea mgogoro huo katikati ya show, ambapo alionekana kutetea upande wa Palestina jambo ambalo liliwafanya mashabiki kuinuka na kuondoka.

 Inadaiwa kuwa msanii huyo wa vichekesho alilaani shambulio la kigaidi dhidi ya Islael ambalo lilifanywa na kikundi cha Hamas kisha akachochea kwa kutaka Wapalestina kulipa kisasi.

Chappelle  mwenye umri wa miaka 50 amewahi kuonekana katika filam mbalimbali zikiwemo, The Nutty Professor ilio toka mwaka 1996,  Con Air iliotoka 1997 na A Star Is Born  mwaka 2018.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags