Mashabiki waomba Manara aachiwe huru

Mashabiki waomba Manara aachiwe huru

Mashabiki kutoka katika Tawi la Temboni wameliomba Shirikisho la ‘Soka’ Tanzania (TFF) kumuachia huru aliyekuwa msemaji wa ‘Klabu’ ya Yanga Haji Manara baada ya kufungiwa miaka miwili na ‘faini’ ya milioni 20 kwa kukutwa na hatia ya kumtolea maneno yasiyofaa Raisi wa TFF, Wallace Karia.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Manara ame-share video ikiwaonesha mashabiki wakiomba TFF kumuachi msemaji huyo kwa ajili ya manufaa ya mpira wa miguu nchini, ambapo Manara ametoa shukrani kwa mashabiki hao kwa kuandika,

“Asanteni Wananchi wenzangu na wanachama wa hili Tawi la Wakali wa Temboni, ni Upendo mkubwa kwangu na kwa football, imenifariji sana na always Wanayanga mmesimama na mimi na kila ninapokwenda kote nchini na hata nje ya nchi, ninapokutana na Wananchi mnanipa heshima na upendo mkubwa.

Ila niwaambie kitu Wakati wa Mungu ni Wakati sahihi, akiandika siku moja mtasheherekea Return of Bugati Insha'Allah”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags