Mashabiki wamtaka Alonso Liverpool

Mashabiki wamtaka Alonso Liverpool

Baada ya ‘kocha’ #XabiAlonso kuiwezesha ‘klabu’ ya #BayerLeverkusen kuifunga ‘timu’ ya BayernMunich, mabao 3-0, jana Jumamosi kwenye ‘Bundesliga’, mashabiki wa ‘klabu’ ya #Liverpool wameweka wazi kuwa wanahitaji kuona ‘kocha’ huyo anachukua nafasi ya #JurgenKlopp ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu ‘klabuni’ hapo.

Alonso ambaye kwa sasa anaifundisha Leverkusen ameiwezesha ‘timu’ hiyo kukaa kwenye kilele cha ligi ya Ulaya ‘Bundesliga’ ikiwa na pointi 55 mbele ya Munich yenye pointi 50.

Kupitia kupitia ukurasa wa X mashabiki wa #Liverpool wametoa maoni yao ya kumtaka Alonso baada ya ukurasa huo ku-share video iliyokuwa ikimuonyesha anashangilia ushindi huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags