Mashabiki wajeruhiwa uwanjani

Mashabiki wajeruhiwa uwanjani

Mashabiki 11 wa ‘soka’ wamejeruhiwa baada ya fataki kurushwa wakati wa ‘mechi’ ya #Bundesliga kati ya ‘klabu’ #Augsburg na ‘klabu’ Hoffenheim nchini Ujerumani, siku ya jana.

Kwa mujibu wa Polisi, fataki hiyo ilirushwa kutokea upande wa uwanja wa WWK Arena, kelele kubwa ilisikika uwanjani hapo huku watu kadhaa wakijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.

Kutokana na tukio hilo mchezo ulisimamishwa wakati wa huduma za dharura zikitolewa na baadaye mchezo uliendelea na kuishia kwa matokeo ya 1-1.Polisi wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na washukiwa wawili tayari wamekamatwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags