Mashabiki wachukizwa na Drake kupaka rangi kucha

Mashabiki wachukizwa na Drake kupaka rangi kucha

Rapa kutoka nchini Canada Drake amekutana na masimango kutoka kwa mashabiki wake, kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa amepaka rangi ya njano na bluu kwenye kucha za vidole.

Hali hiyo imesababisha dhihaka mtandaoni, na kuambiwa sio utamaduni ambao wasanii wa Hip Hop wanatakiwa kuufanya.



Mkali huyo wa Toronto aliamua kuonesha mtindo wake huo mpya mwishoni mwa wiki lakini mashabiki wake hawakufurahishwa sana na suala hilo.

Japo kuwa yeye si mwanamuziki wa kwanza kupaka rangi isiyokuwa ya asili kwenye kucha zake, kwani Tyler The Creator, A$AP Rocky, Kid Cudi, Lil Nas X na hata Machine Gun Kelly tayari wamewahi kuutumia mtindo huo, lakini kwa upande wake na mashabiki zake wamelichukulia ndivyo sivyo jambo hilo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags