Mashabiki wa Dortmund warusha dhahabu bandia uwanjani

Mashabiki wa Dortmund warusha dhahabu bandia uwanjani

Mashabiki wa ‘Klabu’ ya Borussia Dortmund walifanya maandamano katika ‘mechi’ ya Dortmund dhidi ya Newcastle iliyochezwa usiku wa kuamkia leo kwa kurusha pesa na dhahabu bandia uwanjani na kupelekea mchezo huo kusimama kwa muda.

Licha ya kutupa pesa hizo bandia waliweka mabango yaliyokuwa yameandikwa “Hamjali kuhusu soka mnachothamini ni pesa tu” huku vyombo vya habari nchini humo vikieleza kuwa huenda kauli hiyo ni kutokana na mashabiki kupinga mipango ya UEFA kutaka kutambulisha mfumo mpya kwenye ‘Ligi’ ya Mabingwa kuanzia msimu wa 2024-25.

‘Mechi’ hiyo ilitamatika kwa bao 2-0 ambapo klabu ya Dortmund kuondoka na alama zote tatu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post