Mashabiki: Cardi B kudai talaka sio akili zake ni mimba

Mashabiki: Cardi B kudai talaka sio akili zake ni mimba

Usiku wa jana Agosti 1, ‘rapa’ wa Marekani Cardi B kupitia ukurasa wake wa Instagram ali-share picha na kutangaza kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa tatu, jambo ambalo liliwaibua mashabiki wakidai kuwa ‘rapa’ huyo kudai talaka sio akili zake.

Katika posti hiyo baadhi ya mashabiki na wadau mbalimbali walijitokeza kupitia upande wa ‘komenti’ wakidai kuwa kufungua shauri la kudai talaka Mahakamani kwa mumewe Offset huenda ni ujauzito unamsumbua na sio kwa akili zake kwani hapo awali aliwahi kudai talaka lakini wawili hao walirudiana tena, huku wengi wao wakitoa pongezi za kutarajia kupata mtoto wake wa tatu.

Utakumbukwa kuwa kabla ya masaa machache Cardi B kutangaza kuwa ni mjamzito Tmz ililiripoti kwamba‘rapa’ huyo amefungua shauri Mahakamani akidai talaka, hii ni baada ya picha za kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa kwenye huba zito na mpenzi wake wa zamani.

Cardi B na Offset walifunga ndoa mwaka 2017 na wamebarikiwa kupata watoto wawili ambapo ni ‘Kulture’ na ‘Wave’ endapo mimba hiyo itakuwa ya Offset basi atakuwa ni mtoto wao wa tatu pamoja, kwani mpaka kufikia sasa Cardi hajatangaza mwenye ujauzito huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Cardi kudai talaka kwani mwishoni mwa mwaka jana alidai talaka lakini baada ya mwezi mmoja kupita wawili hao walirudiana tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags