Marufuku kupiga muziki kwenye mabanda ya sabasaba

Marufuku kupiga muziki kwenye mabanda ya sabasaba

Oooooh! Kumekucha kumekucha unaambiwa hata kama muziki ni burudani, lakini ndani ya mabanda kwenye maonyesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam maarufu Sabasaba umepigwa marufuku.

Awali baadhi ya mabanda yalikuwa yakipiga muziki, ingawa leo Tan Trade imetangaza kupiga marufuku.

“Hairuhusiwi kupiga muziki, atakayebainika kupiga muziki ndani ya banda la maonyesho utachukuliwa hatua, hilo ni kosa na sheria zitachukuliwa dhidi ya atakayebainika, Tan Trade itakuwa inapita kukagua muda wote kwenye mabanda” hilo ni tangazo la Tan Trade kwenye maonyesho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags