Marioo: Paula kakubali kubadili dini

Marioo: Paula kakubali kubadili dini

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Marioo amefunguka ishu ya kufunga ndoa na mzazi mwenzie Paula Kajala, kwa kuweka wazi kuwafanya hivyo hivi karibuni kwani Paula amekubali kubadili dini.

Marioo ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano yake na Wasafi baada ya kuulizwa swali kuhusiana na wao kuingia kwenye ndoa pamoja na nani atabadili dini kumfuata mwenzake.

“Sisi hapa tunatarajia kuoana, kwa sasa bado hatujaoana, bado tunaishi kihuni lakini tutaoana na Paula ndiyo atabadili dini atakuwa muislamu” amesema Marioo

Mbali na hayo amefunguka kuhusiana na mzazi mwenzae kutokujihusisha sana na mitandao ya kijamii na kudai Paula ameamua kufuata misingi yake.

“Siku zote linapokuja suala la watu kuwa kwenye mahusiano serious kabisa ina maana kuna mmoja ameenda kwenye misingi ya mwenzie, kwa hiyo yeye ametoka maisha yake ya zamani amekuja kwenye misingi yangu na ndiyo maana ametulia. Nafikiri tumekubaliana wote kwa pamoja na amefanya kwa sababu ya upendo tu” amesema Marioo

Ikumbukwe kuwa mahusiano ya Marioo na Paula yalianza April, 2023 ambapo ndani ya uhusiano wao wamebahatika kupata mtoto wa kike aitwaye ‘Amarah’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags