Marioo na Paula wapata mtoto wa kike

Marioo na Paula wapata mtoto wa kike

Baada ya kuthibitisha kutarajia kupata mtoto, hatimaye mwanamuziki Marioo na mpenzi wake Paula Kajala wamepata mtoto wa kike waliyompa jina la Amarah.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Marioo ame-share video akiwa na mtoto wake huyo iliyoambatana na ujumbe

“Asante Mungu kwa Baraka hii ya Mtoto,Tunakushukuru kwa Mtoto wetu wa Kwanza, Our beautiful Daughter Princess Amarah Mungu akukuze akujaalie Afya na Baraka Tele asante Malkia wangu Paula Kajala unastahili kila kilichopo ndani ya uwezo wangu , mungu akubariki sana”

Aidha kupitia video hiyo mastaa mbalimbali walimpongeza msanii huyo kupitia upande wa ‘koment’ akiwemo Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, Lamata, Billnass, Maua Sama na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags