Marekani yaruhusu vidonge vya kutoa mimba kuuzwa madukani

Marekani yaruhusu vidonge vya kutoa mimba kuuzwa madukani

Kwa mara ya kwanza maduka ya dawa ya rejareja nchini Marekani yanaweza kuuza vidonge vya kutoa mimba, chini ya mabadiliko ya sheria mpya na utawala wa Biden.

Watu wanaweza kupata vidonge vya kutoa mimba vya (mifepristone) ambayo ni salama na vyenye ufanisi katika kutoa mimba kutoka kwa mtoa huduma wa afya.

Maelezo ya matumizi bado yanahitajika chini ya sheria mpya, lakini wanao hitaji sasa wanaweza kuchukua vidonge hivyo dukani au kutumiwa kwa njia ya barua.

Hatua hiyo inaweza kuongeza kasi ya utoaji mimba kwa kutumia dawa.

Vidonge vya kutoa mimba vimekuwa vikitafutwa zaidi kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu wa mwaka jana uliobatilisha haki ya shirikisho ya kutoa mimba, huku mataifa kadhaa yakipiga marufuku au kuzuia vikali upatikanaji wa utoaji mimba.

Zaidi ya nusu ya utoaji mimba nchini Marekani tayari unafanywa kwa tembe badala ya upasuaji, kulingana na Taasisi ya Guttmacher inayounga mkono.

Mwezi Disemba mwaka 2021, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) ilisema itaondoa kabisa hitaji la wagonjwa kupata dawa kibinafsi kupitia mtoa huduma ya afya, kama sehemu ya hatua yake inayotokana na janga.

Siku ya Jumanne, FDA ilitoa taarifa mpya katika tovuti yake na mahitaji mapya, ikisema dawa hiyo "inaweza kutolewa na maduka ya dawa yaliyoidhinishwa au chini ya usimamizi wa daktari aliyeidhinishwa".

Danco Laboratories na GenBioPro, kampuni mbili za Marekani zinazotengeneza dawa hiyo, zilithibitisha kwa taarifa tofauti kwamba wakala huo ulikuwa umewafahamisha kuhusu uamuzi wake.

Hatua hiyo imesifiwa kama hatua muhimu mbele na Chuo cha Madaktari wa uzazi cha Marekani na Madaktari wa Magonjwa ya Wanawake.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags