Mapya yaibuka tukio la Tory Lanez kumpiga risasi Megan

Mapya yaibuka tukio la Tory Lanez kumpiga risasi Megan

Wakati ‘rapa’ Tory Lanez akiendelea kutumikia kifungo chake baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia kwa bunduki aliyekuwa mpenzi wake Megani, ripoti mpya zinaeleza kuwa huenda mwanamuziki huyo hakuhusika na kumpiga risasi Megani.

Kwa mujibu wa nyaraka mpya zilizofikishwa Mahakamani dereva wa Tory aitwaye Jauquan Smith ametoa ushahidi juu ya tukio hilo kwa kudai kuwa hakumuona aliyefyatua risasi lakini rafiki wa Megani, Kelsey Harris alionekana akitoka bunduki.

“Risasi ilifyatuka ghafla wakati Tory, Megan na Kelsey walipokuwa wakigombana lakini sikumuona aliyefyatua risasi hiyo” amesema Jauquan Smith

Utakumbuka kuwa mwanzoni mwa kesi hiyo shuhuda mmoja alidai kuwa aliyefyatua risasi katika mzozo wa watatu hao alikuwa ni mwanamke lakini jina lake halikuwahi kuwekwa wazi hadi leo.

Licha ya ushahidi huo kutolewa, mahakama haikupokea ushahidi huo kwani hapo awali mawakili wa Tory waliwahi kumkataa Smith kuwa shahidi wa kesi hiyo.

‘Rapa’ Tory Lanez anatumikia kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu (kushambulia kwa kutumia bunduki, kubeba bunduki ambayo haijasajiliwa, na mengineyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags