Mapenzi chanzo Tiwa kuingia kwenye muziki

Mapenzi chanzo Tiwa kuingia kwenye muziki

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria #TiwaSavage ameweka wazi kuwa aliingia kwenye muziki kwa sababu ya mwanaume, lakini ndoto yake ilikuwani uigizaji.

Tiwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumzia ujio wa filamu yake mpya ya ‘Water and Garri’ ambapo alidai kuwa uigizaji ulikuwa ni moja ya ndoto yake na wala haiingilii fani za watu wengine kama baadhi ya watu wanavyosema kupitia mitandao ya kijamii.

Aidha alieleza kuwa aliingia kwenye muziki kwa sababu ya mapenzi, mwanaume aliyekuwa naye hapo awali alikuwa anapenda muziki ndipo akaamua kuachana na kuigiza na kugeukia kwenye muziki ili kumfurahisha mpenzi wake.

‘Water and Garri’ ni filamu ambayo inasimulia maisha halisi ya mwanadada Aisha (Tiwa) ambaye ni mbunifu wa mavazi aliyetumia miaka 10 nchini Marekani ambapo inambidi arudi nyumbani kwao kwa ajili ya msiba wa mmoja wa familia yake lakini anakuta maisha ya nyumbani kwao yamebadilika vurugu zimeongezeka.

Ikumbukwe kuwa filamu hiyo ya ‘Water and Garri’ inatarajiwa kuachiwa rasmi Mei 10 mwaka huu, ambapo itaruka kwa mara ya kwanza kupitia Prime Video.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags