Mapacha wazaliwa miaka tofauti

Mapacha wazaliwa miaka tofauti

Katika hali isiyo ya kawaida, watoto wa kike mapacha kutoka nchini Croatia watasherehekea siku ya kuzaliwa kwa tarehe na miaka tofauti baada ya kupishana dakika moja.

Mapacha hao ambao walizaliwa usiku wa mkesha wa mwaka mpya Disemba 31 ambapo pacha mmoja alizaliwa saa 5:59 usiku, huku wapili akizaliwa saa 06:00 Januari 1 katika hospitali ‘Split University Hospital’.

Mkuu wa idara ya perinatology hospitalini hapo Damir Roje alitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari vya ndani akieleza kuwa ni hali isiyo ya kawaida kwani amezoea kuona mapacha wakizaliwa siku tofauti lakini siyo miaka tofauti na hiyo ndiyo mara yake ya kwanza kushuhudia katika taaluma yake.

Tofauti hiyo ndogo inamaanisha kuwa familia ya mapacha hao itasheherekea siku mbili za kuzaliwa kwa watoto wao ambapo wa kwanza atasheherekea usiku wa mwaka mpya na mwingine katika mwaka mpya, Januari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags