Mapacha waliozaliwa miaka tofauti

Mapacha waliozaliwa miaka tofauti

Imezoeleka kuwa mapacha wengi uzaliwa siku moja na mwaka mmoja, lakini kwa mapacha hawa Afredo na Aylin kwao ni tofauti hawakuzaliwa tuu kwa siku tofauti lakini pia mwaka tofauti.

Tukio hili limewashangaza wengi ambalo limetokea California nchini Marekani mwana Mama Fatima Madrigal aliyejifungua mapacha wawili waliopishana dakika 15, mmoja alizaliwa mwaka 2021 na mwingine 2022.

Fatima Madrigal na Robert Trujillo walipata mtoto wa kiume December 2021 saa 5:45 usiku aliyepewa jina la Afredo na baada ya dakika 15 ambayo ilikuwa saa 6 usiku ambayo ni siku nyingine ya mwaka mpya wa 2022 walipata mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Aylin.

Watoto pacha hawa watakuwa wakisherehekea siku zao za kuzaliwa miaka tofauti sababu ya mwanya wa dakika 15 katika kuzaliwa kwao.

Hii ina maana kuwa Alfredo na Aylin ni pacha lakini walizaliwa mwezi, siku na mwaka tofauti.

Amaah kweli Mungu anamaajabu yake, usisahau kulike na kudondosha comment yako hapo chini utupe maoni yako juu ya hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags