Maombolezo siku 14 baada ya kimbunga freddy kuua watu 225

Maombolezo siku 14 baada ya kimbunga freddy kuua watu 225

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza siku 14 za maombolezo baada ya kimbunga freddy kuuwa zaidi ya watu 225.  pia ameagiza Bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku 7.

Aidha ameendelea kwa kueleza kuwa mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri umeidhinisha kutolewa Tsh. Bilioni 3.5 kwaajili ya kusaidia maelfu ya wananchi walioathirika.

Hadi sasa zaidi ya watu 19,000 wamepoteza makazi na wengine hawajulikani walipo kutokana na athari za kimbunga freddy

Umoja wa Mataifa (UN) umetuma msaada wa vifaa ikiwa ni pamoja na usafiri kwaajili ya shughuli za utafutaji na uokoaji, vifaa tiba, usambazaji wa chakula, maji na mahema


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post