Maokoto yambadilisha Rihanna, ajifunga mtandio kiunoni

Maokoto yambadilisha Rihanna, ajifunga mtandio kiunoni

Mwanamuziki Rihanna amewashangaza wengi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa nchini India amejifunga mtandio kiunoni.

Rihanna ameonekana kwenye vazi hilo wakati akitoka kuongea na bilionea Mukesh Ambani kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tafrija ya sherehe ya harusi ya kijana wake Anant Ambani inayotarajiwa kufanyika wiki hii.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa Rihanna amelipwa mpunga mrefu kwa ajili ya kutumbuiza kwenye sherehe hiyo ambapo inadaiwa kuwa amelipwa dola 9 milioni, ambazo ni zaidi ya tsh 22 bilioni.

Hii siyo mara ya kwanza kwa bilionea huyo kuwaita wanamuziki wakubwa kutumbuiza katika sherehe za harusi za watoto wake, mwaka 2018 alimlipa mwanamuziki Beyonce kutumbuiza kwenye harusi ya binti yake Isha Ambani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags