Mwigizaji maarufu kutoka Marekani Robert Downey Jr anatajwa kuwa mwigizaji aliyevuna mkwanja mrefu katika kampuni ya Marvel (Marvel Cinematic Universe MCU) kufuatia na uhusiaka wake wa Iron Man.
Kwa mujibu wa tovuti ya Forbes mwigizaji huyo anatajwa kwenye orodha ya waigizaji wanaolipwa zaidi dunia ambapo katika uhusika wake kwenye filamu zote akicheza kama Iron Man ameingiza zaidi dola milioni 500 sawa na Sh 1.3 trilioni.
Akianzia na mshahara wa kawaida katika filamu ya kwanza ya Iron Man 1 alilipwa dola milioni 1, Iron Man 2 akiingiza dola milioni 10, The Avengers akilipwa dola milioni 50, Iron Man 3 akiondoka na dola milioni 50 pia, Avengers: Age of Ultron akipata dola milioni 80, Captain America: Civil War dola milioni 64.
Spider-Man: Homecoming akipata dola milioni 15, Avengers: Infinity War dola milioni 75 milioni, Avengers: Endgame akipata dola milioni 75 pia, Avengers; Doomsday akilipwa dola milioni 80. Hata hivyo inaeleza kuwa malipo hayo yanatokana na Mshahara pamoja na mgao wa faida kutokana na mafanikio makubwa ya filamu.

Leave a Reply