Mandonga mtu kazi apata dili nono, Kigoma

Mandonga mtu kazi apata dili nono, Kigoma

Nyie nyie ama kweli nimeamini kila mja na nyota yake bwana, lakini kwa bondia huyu naona yake inazidi kuwaka kila siku, bondia maarufu nchini Karim Mandonga ambae alipata umaarufu huo baada ya kuchapwa na bondia mwenzie Shaban Kaoneka, juzi aliyekwenda Kigoma kwa ajili ya mpambano wake amelazimika kuahirisha safari yake ya ndege kurejea Dar es salaam  baada ya uongozi wa Mkoa wa Kigoma kumpa dili nono la kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana Kigoma.


Mandonga amepata mwaliko wa kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Esther Mahawe na Katibu Tawa wa Mkoa huo ambapo Viongozi hao wamempongeza Bondia huyo kwa juhudi anazozionesha katika michezo yake.

Mandonga amesema anamshukuru sana Mungu kwa fursa aliyompatia ya kufahamika baada ya kupigwa na Bondia Shabani Kaoneka ambapo amesema Kaoneka ni kama amemfungulia njia ya kupata mafanikio katika maisha yake.

“Kaoneka amenipa maisha yenye msingi, kusema ukweli nilionao moyoni na sijapinga kwamba pambano lile sikupigwa na Kaonekana eti kwasababu sijui kupigana ila alinizidi ujanja akabahatisha kunipiga sehemu nyeti nikapoteza mchezo kiuhalali lakini nataka kurudiana nae ili nimuoneshe kuwa Mimi sio Mtu wa mchezomchezo, akitaka hata kesho turudiane Mimi niko tayari na wala hatonipiga tena” amesema Karim Mandonga

aidha Mandonga aliendelea kwa kusema kuwa “Kwa madili yangu haya ninayopata nina vitu nataka kuvipata ili kutimiza ndoto zangu, nilikuwa naishi kwenye kibanda kwahiyo natamani kupata nyumba nzuri na usafiri wa gari aina ya Jeep napigana sana kutimiza haya” amesema Mandonga mtu kazi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags