Mandojo kuagwa leo Dodoma, kuzikwa kesho Manyoni

Mandojo kuagwa leo Dodoma, kuzikwa kesho Manyoni

Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva, Joseph Frank maarufu Mandojo anatarajiwa kuzikwa kesho eneo la Samaria, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Mandojo alifariki dunia Jumapili Agosti 11, 2024 wakati akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Msemaji wa familia na mdogo wa marehemu, Yohana Chacha amesema leo Agosti 13, 2024 kuwa wanakwenda hospitali kuchukua mwili wa mpendwa wao leo kwa ajili ya kuaga Ndachi.

"Sasa hivi tunaelekea Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuuchukua mwili na baadaye tutakwenda nyumbani kwa ajili ya kuuga," amesema Chacha.
Amesema mwili huo utasafirishwa leo kwa ajili ya mazishi wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

Kwa mujibu wa Chacha, kaka yake hakurejea nyumbani kwa mkewe Nzuguni jijini Dodoma tangu alipoondoka Jumamosi Agosti 10, 2024, hali iliyowafanya ndugu kumtafuta.

Chacha amesema katika jitihada za kumtafuta walimkuta katika kituo cha kati cha polisi na aliwaomba wampeleke hospitali lakini alipopelekwa alifariki dunia muda mfupi akiwa katika idara ya wagonjwa wa dharura.

(Imeandikwa na Sharon Sauwa)






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags