Manchester City yafuzu michuano ya FA CUP

Manchester City yafuzu michuano ya FA CUP

Mambo ni moto mambo ni fire!! Watoto wa mjini wanasema hivyo bwana sasa basi iko hivi Timu za Manchester City, Middlesbrough na Crystal Palace zimefuzu hatua ya robo fainali ya michjuano ya kombe la FA CUP nchini England baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya 16 bora jana Usiku, huku Tottenham ikitupwa nje ya mashindano.

Mabingwa mara 6 wa michuano hii Manchester City wamefuzu robo fainali baada ya kuinyuka Peterborough mabao 2-0, mabao ya City yamefungwa na Riyad Mahrez aliyefunga bao lake la 19 msimu huu kwenye michuano yote na bao la pili limefungwa na Jack Grealish, Crystal Palace wao wameitoa Stoke City kwa kuinyuka kwa mabao 2-1, kwenye mchezo uliochewa katika dimba la Selhurst Park London mabao ya ushindi ya Palace yamefungwa na Cheikhou Kouyate na Jairo Riedewald lile la kufutia machozi la Stoke limefungwa na Josh Tymon.

Middlesbrough ya Championship wameitoa Tottenham Hotspurs kwa kuifunga bao 1-0 bao lilofungwa dakika ya 107 na kinda Josh Coburn mwenye miaka 19, mchezo huu ulichezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumaliza kwa Suluhu hivyo dakika 30 za ziada zikaongezwa.

Michezo ya raundi ya 5 ambayo ni sawa na hatua ya 16 bora inaendelea tena leo ambapo itachezwa michezo 3, mchezo wa mapema ni Saa 4:15 usiku Luton Town wataminyana na Chelsea , Saa 4:30 Watakatifu Southampton wanacheza na wagongwa nyundo wa jiji la London West Ham United. Na mchezo wa mwisho unachezwa saa 5:15 Usiku ambapo Liverpool watakipiga dhidi ya Norwich City.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags