Manara: kwaheri Fiston Bugati Mayele

Manara: kwaheri Fiston Bugati Mayele

Baada ya wachezaji na baadhi ya viongozi kumtakia kheri mchezaji Fiston Mayele, hatimaye aliyekuwa msemaji wa ‘klabu’ ya #Yanga Haji Manara naye ametoa baraka zake kwa #Mayele  baada ya kusajiliwa na ‘klabu’ ya Pyramid kutoka nchini Misri

Kupitia Instagram yake Manara ame-share video akitoa baraka zake kwa mchezaji huyo. Manara amesema,

“Fiston katika misimu miwili ametufungia ma’goli’ zaidi ya 50, kusema ukweli nikimtaja Fiston, achana na perfomance yake ndani ya peach ni binadamu sana ni mtu mpole, mcheshi na anasifa zote, mimi nam-miss kama rafiki na streak, niwaambie tunampoteza mchezaji mkubwa, ila #Yanga haiwezi kusema itatetereka, itam-miss

Kupata quality ya Mayele ni changamoto sana lakini kwa sababu tumejipanga na tulikuwa tumejiandaa ‘kisaikolojia’ hivi kuna mchezaji star Tanzania kushinda Mayele mbona hakukuwa na mizengwe kaja muungwana Pyramid wameleta mzigo mzito, tuna fedha tunaweza kununua wachezaji wote hawa mpata mpatae tukawasajili tukawapeleka feri wakatusaidie kuvua samaki

Kuna siku ningetamani Yanga tucheze na Pyramid Mayele pale akutane na wanaume sasa wakina Mwamnyeto, Bacca, Mayele anajua alikuwa anakutana na mtu anaitwa Bacca mazoezini kila siku alikuwa anataka kurusha ngumi Ibrahim Bacca alikuwa anakosha akipanda juu wanaenda wote wakishuka wanashuka wote anamwambia hapa umayele kule Mkapa hapa Avic mimi ndo Mayele

Manara alimalizia kwa kusema kwaheri mwamba na kila la kheri katika maisha yako mapya Fiston Kalala Bugati Mayele”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags