Man United yawataka Cunha na Kudus kwa mpigo

Man United yawataka Cunha na Kudus kwa mpigo

‘Klabu’ ya Manchester United imepanga kutumia Pauni 60 milioni kwenye usajili wa straika wa Wolves, Matheus Cunha huku ikiweka mipango yake sawa kumnyakua pia staa wa West Ham United Mohamed Kudus ambaye amekuwa kwenye ubora wa hali ya juu msimu huu.

Straika Cunha kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Man United tangu alipokuwa Atletico Madrid kabla ya kwenda Wolves na huenda akabadili timu kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya hivi karibuni kusema kuwa anataka kupata changamoto nyingine.

Hata hivyo, imekuwa ikielezwa kuwa staa huyo anataka kucheza kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao na nafasi hiyo anaweza kuipata endapo atajiunga na Man United.

United inahitaji saini ya Cunha kama atakuwa anapatikana sokoni kwa sasa, huku Kudus akiwemo kwenye orodha ya mastaa ambao timu hiyo inataka kwenda nao kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Kudus mwenye miaka 23 amefunga mabao 14 kwenye michezo 44 aliyoichezea timu hiyo ya London.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post